Breaking News

VICHEKESHO NA ISUBA MEN

1. BABA:"Mbona unafeli kila mtihani mwanangu?"
MTOTO:"Sababu sina akili."
BABA:"Ooh,sasa ngoja nikupige fimbo za kutosha ili
uwe na akili mshenzi
wewe!"
MTOTO:"Ingekuwa fimbo ndio
humfunza mtu kuwa na akili,basi punda
na farasi wangekuwa MAPROFESA."





2. Watoto wawili walirudi kwao na
majibu ya mtihani wa mwisho wa
muhula;
BABA:"Safi sana naona umepata
A katika masomo yako yote." Diana unataka zawadi gani?
DIANA:"Nataka kwenda kusoma AUSTRALIA."
BABA:"Na wewe Tina naona
umepata E masomo yote! Ndo
nini hii?"
TINA:"Nataka kwenda kusoma
England!"






3. father ; nilete soda we mtoto
son ; pepsi au  coka?
father ; pepsi
son ; ya kopo au ya chupa? father ; ya kopo
son ; ya baridi or ya moto?
father ; hee! we mtoto mbna maswali mengi....basi
bwana ni letee maji tu
son ; ya hapa hom or nika nunue kwa shop?
father ; ya hapa hapa
son ; ya baridi ya moto? father ; ya baridi

son ; kwenye glasi or kikombe?
father ;
ntakupiga na ufagio we mtoto
son ; ufagio wa chelewa or wa mti?
father ; ntaku uwa we mtoto
son ; uta uwaje utanichoma kisu or utanipiga na
bastola?
father ; ntakupiga na bastola
son ; kichwani or tumboni?
father ; kichwani...NIMEKWAMBIA TOKA NJE son ; sasa hivi or baadae kidogo?
father ; sasa hivi
son ; maji hutaki?



Mume: Hello baby!
Mke: Hello swt!
Mume: Nitachelewa kurud leo
Mke: Nishajua uko kwa vijanamke vyako, ww ni mzinzi sana cjui ilikuaje ukanioa nakuchukia kama nn? ckupend! ckupend!
Mume: Niko BENKI hapa
Mke: Haa! Ulijuaje kama cna hela, nitolee laki 1 baby, nakupenda sana kuliko roho yangu, nakutengea maji yakuoga sweety. Ucsahau hizo pesa ninunulie na chips kuku mmwaaaa!
Mume: Ni BENKI YA KUCHANGIA DAMU
Mke: Nyoooo waambie wakutoe yote
 Mwalimu mmoja wa shule zetu kama nilizosoma mimi shule za msingi yani alimuagiza mwanafunzi wake akichanganya lugha ya kiswahili na kiingereza...... MWALIMU; we Evarist nifatie stick nimtandike huyu John MWANAFUNZI: mwalimu sasa hapa ni mbali na dukani ntazipata wapi hata hela hujanipa MWALIMU: nimesema lete stick alaaa BASI MWANAFUNZI AKAKIMBIA NYUMBANI KWAO KUCHUKUA STICK ZA KUCHOKONOLEA MENO........ BAADA YA MUDA KAMA DK 30 AKARUDI SHULE ......MWALIMU: enhee we ulifata mpaka wapi na mbona hujaileta MWANAFUNZI: mwalimu nyumbani ni mbali sana lakini hata hvyo mama kanipa haka kapakti kazma...... MWALIMU AKASHNDWA HATA KUMCHAPA
 Hii ni english ya mwanafunzi bora wa form 4 kutoka shule mojawapo za kata TZ akimwambia mzungu ugumu wa kupanda mlima k/njaro sababu njia haijanyoka moja kwa moja:
SIR, TO PLANT MOUNT KILIMANJARO IS NOT A PRESIDENT JOB BECOZ THE WAY IS NOT SNAKE ONE BY ONE. Tanzania inakwenda wapi??
Kuna jamaa mmoja alikuwa mlevi sana wa pombe aina ya gongo.Mke wake na majirani zake walikuwa hapendi tabia yake ya kulewa mpaka anapoteza network.Hata hivyo mke wake kwa kushirikiana na majirani walifanikiwa kumshawishi aachane na kunywa gongo.Jamaa baada ya kutumia ulevi wa kienyeji,baadhi ya siku huenda Bar kunywa bia.Habari hizi zikamfikia mkewe.Mke akaumuuliza mumewe nasikia umeshanza kulewa tena?Jamaa akamjibu mkewe "Pele alisitaafu kucheza mpira lakini danadana anaruhusiwa kupiga.Kwa hiyo mimi niliacha kunywa gongo,lakini baadhi ya siku naenda Bar kupata bia."
 Siri Baba: mwanangu, enhe shika hii 500Tsh usimuambie mama yako kuwa nimelala na housegirl. Mtoto: sitaki, tatizo we baba ni mbahiri sana mwenzio mama akilala na dereva ananipaga 1,000Tsh. 

Mchaga. Mchaga alipata ajali alipozinduka pale hospitali akauliza "nipo wapi hapa?" Nesi akajibu,"umepata ajali, hapa upo hospitali. Bahati mbaya umekatika mkono." Mgonjwa: Na je saa yangu ipo wapi ya Rolex? Ipo mzee, nesi alijibu. Nesi: Mkeo na watoto wapo hapa kukufariji. Mgonjwa: Yeuwi... Wamefunga duka? 
  
Kimombo na sms Jamaa katumiwa msg na dem wake,kutokana na urefu wa msg ikashindwa kufika yote mwishoni ikaandika'some text missing'jamaa kizungu hajui hivyo maneno ya mwisho hakuelewa maana yake lkn akahisi litakuwa neno la kimahaba,kusudi aonekane mjanja akajibu, "some text missing too dear"
 Mlevi alirudi home na kumkuta mkewe akiwa katika bikini moja matata
Kinyume na mategemeo ya mke aliyekusudia kuamsha usiku wa malove-davi, mlevi akacheka mpaka mke akashangaa

Mke: mume wangu kinachokuchekesha ni nini?
Mlevi: unajua mke wangu toka nizaliwe sijawahi ona t'ako limevishwa kandambili
 Msikie mwehu huyu alienda kwa rafiki yake kupiga story, mara mvua kubwa ikanyesha mshkaji akabidi amwambie rafiki yake usijali utalala hata hapa sebuleni kwa kuwa mvua kubwa! jamaa akasema poa Nitalala usijali.! mwenyeji alipoingia chumbani kwake kulala kama dakika kumi akatoka chumbani akamkuta rafiki yake amelowa chapachapa alipomuuliza vipi mbona hivyo.? Jamaa akajibu .....Nilienda kuchukua shuka nyumbani..!
 Dada mmoja alikuwa bafuni akioga,mara akasikia hodi ikipigwa mlangoni,akajibu karibu huku akijisetiri kwa taulo na kanga ili akampokee mgeni.Alipofungua mlango,akakutana uso kwa uso na kijana mmoja kipofu aitwaye John,akamkaribisha kiti,kwa sababu anajua John ni kipofu,akavua taulo lake na ile khanga,akachukua mafuta ya lotion akaanza kujipaka kwa mbwembwe na pozi za kila aina.
"Enhee rafiki yangu john,nambie,kuna jipya?umeadimika saana rafiki yangu.John akamjibu,"yaap ni kweli niliadimika saana kwasababu nilikuwa China kufanyiwa operation ya macho na sasa nina uwezo wa kuona vizuri kabisa,kwa hiyo lengo la kuja hapa ni kukualika uje katika sherehe niliyoiandaa kujipongeza kwa operation kwenda vyema.
SWAGA ZA WADADA ZETU ILI WAONEKANE NAO WAMO HASA WAKITOKA USWAZI WAKAWA WAMENDA OUT MITAA YA USHUANI;;;
1. Halima………muhudumu naomba unilete salad ya moto, na chupa ya Amarula.

2. Chausiku…..nipe PIN yako niwe nakupigia

3. Siwema….nimechokaje, nimeshinda Shoprite natengeneza nywele

4. Gulo….Boifrend wangu kanambia likizo ya summer mwaka huu London nikale Chrismas

5. Cynthia…Nimenunua BlackBerry wamenambia PIN nikaipitie kesho

6. Fulo....Mi napendaga kusafiri na Presishen, napenda viti vya dirishani, mtu unakaa unafungua kioo chako hewa safiii mpaka mwisho wa safari.:p

7. Fatu….kiukweli mi niliipenda London kuliko Uk
Mtoto alimuuliza baba yake eti baba ukikuta noti ya sh.10,000 na sh. 5,000 utaokota ipi? Baba akajibu we ----- nini? Naokota ya sh. 10,000. Mtoto: We ndo -----! mimi naokota zote!!!
Kuna majambazi walifanikiwa kuingia Bank na kuiba Pesa nyiingi,na kufanikiwa kutoroka, wakafika sehemu wakaanza kuzihesabu, hadi wakachoka kuhesabu! Mmoja akawambia"Oyaa mi nimechoka,tusubiri taarifa ya habari Itangaze tumeiba Sh Ngapi!