DIAMOND: NILISHAWAHI MKUTA WEMA AKIWA UCHI NA MTU MWINGINE HOTELINI.
Baada
ya kuamua kutokaa kimya kutokana na shutuma zilizotolewa dhidi yake na
mpenzi wake wa zamani WEMA SEPETU, Mwimbaji DIAMOND PLATNUMS ameamua
kutoa kauli yake ya mwisho kuhusu Wema.
Diamond
anakiri kwamba hakutaka kabisa kumzungumzia Wema kwenye vyombo vya
habari baada ya kuachana kwa sababu hakutaka malumbano lakini imebidi
iwe hivyo kwa sababu ya hasira aliyoipata kutokana na Wema kuzungumza
uongo mwingi dhidi yake.
Exclusive
na millardayo.com Diamond amekiri kwamba aliachana rasmi na Wema mwezi
january mwaka huu na hiyo ni kutokana na kukerwa na tabia za Wema
alizozikemea lakini mwisho wa siku hakufanikiwa, zikawa zinaendelea….
ambapo tabia hizo ni pamoja na Wema kuwalipa waandishi wa habari wa
magazeti ili watoe stori zake, japo Diamond alikua anawalipa waandishi
wasiandike chochote, yeye alikua anawalipa zaidi.
Diamond
amesema “kuna vitu vya chinichini alikua ananifanyia vya kuniumiza kama
kudanganyana lakini nilikua sivipeleki kwenye vyombo vya habari kwa
sababu nilikua namuheshimu namfichia kwa sababu anasema hafanyi hivyo,
lakini akawa anaendelea kuvifanya kama kunidanganya kwenye mapenzi japo
kudanganyana kwenye mapenzi ni kitu cha kawaida hata wapenzi wangu wa
zamani walikua wananidanganya na mimi nawadanganya pia, lakini alikua
anapeleka kila kitu kwenye magazeti hata vitu vya watu wawili ndani ya
nyumba anavipeleka, sasa nyumba inakua haina siri”
Ameamplfy
zaidi kwamba “Wema alikua anapeleka stori kabisa yani kitu tumefanya
watu wawili ndani unashangaa kukikuta kwenye gazeti, nikikutana na
waandishi ambao ni rafiki zangu wananiambia ebwana wewe unajisumbua bure
yeye mwenzako akija hapa ndio anataka aandikwe, mimi nilishawahi
kumkuta hotelini uchi kabisa akiwa na mwanaume mwingine hotelini
mwishoni mwa mwaka jana lakini sikuongea chochote kwenye vyombo vya
habari, nikamchukua na kuondoka, niliamua kumtunzia siri yake na
nikanyamaza kwa kuichukulia kama mwanaume, na hata nikawa nikifika
kwenye media nilikua nampamba na kumtetea kwamba jamani Wema hayuko
hivyo na ni mstaarabu”
Diamond
amefunga mjadala wa yeye na Wema kwa kuthibitisha kwamba hana ugomvi na
Wema wala hana tena hisia za kimapenzi kwa mshindi huyo wa Miss
Tanzania 2006, hawezi kurudiana nae kwa sababu kwa sasa imetosha na
anampenzi mwingine ambae hata Wema anamfahamu.
Ishu
yote hii imetokana na show aliyoifanya Diamond pale Mlimani City
weekend iliyopita ambapo Diamond alikataa kupokea pesa Wema Sepetu
aliyokua anampa pale kwenye stage kwa sababu ya kukwepa Drama, Na Wema
hakua mpenzi pekee wa zamani wa Diamond aliekuwepo kwenye show, kulikua
na warembo wengine wawili wa zamani wa Diamond lakini hao wote alipokea
pesa zao.
Uhusiano
wa Diamond na Wema umedumu kwa mwaka mmoja ambapo walipanga kuoana huku
tayari Diamond akiwa amemvisha pete ya uchumba mrembo huyo ambae pia ni
mwigizaji wa movie Tanzania.
Diamond
amethibitisha kwamba Show yake ya DIAMONDS ARE FOREVER siku tatu kabla
ya kufanyika, tayari ilikua imeuza ticket zote elfu moja na hivyo ukumbi
kujaa, huku kila ticket ikiwa ni shilingi elfu 50…… show yake imekua
show ya kwanza ya msanii wa kibongo kulipisha watu elfu 50 na bado
ikajaza mapak watu wakakosa ticket, kwa swala la kiingilio amezishinda
mpaka show za Jay Z & 50 cent ambazo zilifanyika bongo na watu
kulipa elfu 25 – 30.
No comments