Breaking News

ROMA AFAFANUA MSTARI UNAOONEKANA KUMDISS JOE MAKINI NA KUSEMA HIYO SIO DISS KWA JOE


 Kupitia top 20 ya Clouds Fm , Roma amefunguka na kutoa ufafanuzi juu ya line iliyoko kwenye ngoma yake mpya 2030 iliyosababisha watu wengi kuuona kama ni diss moja kwa moja kwenda kwa mwamba wa kaskazini Joe Makini.kabla hujamsikiliza alichokizungumza, roma pia alitoa ufafanuzi huo kupitia ukurasa wake wa facebook na hiki ndicho alichokiandika
  
R.O.M.A 2030

HUWEZI KUIJENGA ROMA HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA/
IWE KWA RAHA LEO AU SIMBA MTOTO TANGA WATAKUJA/
HATA PACHO PIA NI MWAMBA ILA BADO ANAKATA VIUNO/
KASKAZINI BILA TANGA NI MSONDO BILA GURUMO/

ALISEMA JUU YA MWAMBA ATALIJENGA KANISA/
NA HALITATIKISIKA WAUMINI TUIANZE MISA!!!

-Ilitumika na inazidi kutumika nguvu na akili na siku nyingi sana kuweza kumjenga R.O.M.A mpaka leo amekuwa hivo alivyokuwa....NA BAAADOOO!!!

-Tanga kuna vingi vizuri(MUZIKI MZURI), wasipokuja kwa hili watakuja kwa lile!! KARIBUNI SANA TANGA MARAFIKI!!!

-Hakuna mkubwa wa wote, unaweza kuwa BINGWA/ NGULI/ MWAMBA/ GAMBERA/ SHUJAA.....
lakini still tukakuona mlaini tu, na haustahili ukubwa huo unaopewa pengine kwa jicho la kawaida tuu!!
pengine kofia uliyojivika kaikustahili(kivitendo zaidi tuonyeshe na tutakubali, isiwe tu kwa maneno!! hata mimi wakati mwingine wananikataaga!! so ni muda wa kuwaprove watu wrong!!!)


Hip hop music miaka mingi na hadi sasa imekuwa ikiongelewa sana na wadau na wasanii na hasa mashabiki kuwa ipo KASKAZINI huku wakiitaja ARUSHA tu!!!

nafurahi kuona ARUSHA ni jiji lenye love na muziki huo na nina mashabiki wengi sana kule!!! lakini napenda kuona TANGA pia ikiongelewa kuhusu muziki huo wa hip hop!!

kwa maana tunae dani msimamo/ wagosi wa kaya/ mwana F.A/ CPWAA/ ROMA na wengine wengi!! na wote wanatumia nguvu nyingi kuutangaza muziki huo, labda tu wanasahau kuutangazia uma kuwa wanatokea/ kuwakilisha TANGA, basi mimi ndiyo nawapasha hayo myajue!!!

na kuna under grounds rapers wakali sana toka TANGA na wote wanaitaka nafasi hiyo!! so haiwezi kuwa kaskazini bila tanga, ilhali tanga nayo imo katika list ya ukaskazini na uhip hop!!!

ni sawa na msondo awepo ROMARIO PEKE YAKE BILA GURUMO INAKUWA HAIJAKAMILIKA!!!

-Ukirudi kwenye vitabu vitakatifu vinasema

JUU YA MWAMBA NITALIJENGA KANISA
NA HALITATIKISIKA!!!!

tukasome vifungu hivo na tutapata upeo wa juu zaidi
Na kisha....TUIANZE MISA

JUMAPILI NJEMA MARAFIKI na MFUNGO MWEMA!!!

Tumsifu yesu kristo!!!
Asalam aleikum!!!
Vruuuuuum TONGWE RECORD BEIB!!!

No comments