Ludacris ashtakiwa kwa kuiba wimbo "Sex Room" mwaka 2009
Rapper kutoka Atlanta, Ludacris ameshtakiwa na msanii emcee Marvo kwa
kuibwa wimbo "Sex Room" aliouachia mwaka 2009. Marvo anadai yeye ndio
alitoka na idea ya kwanza (2009) ya wimbo huo ambao Luda amemshirikisha
Trey Songs.
Kutokana na mtandao wa AOL, Marvo alikuwa akifanya kai na producer
anaeitwa Kajun ambae mwisho wa siku alimgeuka na kumpa wimbo huo
Ludacris, na licha ya kumpa wimbo huo, hajapokea hela yoyote ya malipo
kwa kuutumia wimbo huo, licha ya kuwa Luda ametumia mashairi yake mengi.
Kiasi cha pesa anachokidai bado hakijajulikana
No comments