CHEKA UONGEZE SIKU ZA KUISHI 7
Kuna jamaa mmoja alikuwa mlevi sana wa pombe aina ya gongo.Mke wake na
majirani zake walikuwa hapendi tabia yake ya kulewa mpaka anapoteza
network.Hata hivyo mke wake kwa kushirikiana na majirani walifanikiwa
kumshawishi aachane na kunywa gongo.Jamaa baada ya kutumia ulevi wa
kienyeji,baadhi ya siku huenda Bar kunywa bia.Habari hizi zikamfikia
mkewe.Mke akaumuuliza mumewe nasikia umeshanza kulewa tena?Jamaa
akamjibu mkewe "Pele alisitaafu kucheza mpira lakini danadana
anaruhusiwa kupiga.Kwa hiyo mimi niliacha kunywa gongo,lakini baadhi ya
siku naenda Bar kupata bia."
No comments